Passt nicht? Macht nichts! Sie können Artikel bis zu 30 Tage zurückgeben
Mit einem Geschenkgutschein können Sie nichts falsch machen. Der Beschenkte kann sich im Tausch gegen einen Geschenkgutschein etwas aus unserem Sortiment aussuchen.
Tanzania iliingia katika uchaguzi mkuu ulioshirikisha vyama vingi kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995. Kampeni kubwa za kitaifa na kimataifa zilifanyika hadharani na sirini. Yako mengi yaliyokuwa yakiendelea ,Nyuma ya Mapazia,. Mengi ya kutisha na kuogofya, na ambayo yaliambatana na matumizi makubwa ya pesa, mauaji ya kikatili na ujambazi usio na kifani. Joram Kiango, Inspekta Kombora na kikosi kizima cha polisi wanagonga mwamba katika harakati zao za kutatua kizungumkuti hicho. Kutokweka kwa King Halfan King na maiti ya mpenziwe kupatikana ikielea ufukweni wa Bahari ya Hindi kunazidisha maswali mengi bila majibu. Hata hivyo, kizungumkuti hiki kitatatuliwa?
Hallo! Ich bin Libroamiko, dein Buchberater.
Wie kann ich dir helfen?